Washington, Marekani - 17/04/2012. Wachunguzi wa mambo ya kisiasa
nchini Marekani wametoa matokeo ya utafiti wa kura za maoni wa ugombea
urais ambao unaonyesha rais wa sasa Baraka Obama anaongoza.
Kwa mujibu wa kura hizo za maoni, "Baraka Obama wa chama cha Demokratic
anaongoza kwa 52% na mpinzani wake Mitt Romney wa chama cha Republikan
kupata kura za maoni 43%." na wanacha wa chama Demokratik kudai ya
kuwa Baraka Obama ndiye kiongozi anayefaa kuingoza tena Marekani.
Matokeo hayo yamekuja baada ya mgombea mwenza wa chama cha Republikan
Rick Santorum kujitoa katika kinyang'anyiro cha kugombe kiti cha urais
wa Mareakani na kumwachia nafasi mgombea pekee kupitia chama hicho Mitt
Romney.
Pilika za kutaka kuwania kiti cha urais nchini Marekani zimeshaaanza kwa
mwendo wa gia namba moja tayari kwa kila mgombea kujipanga wakati wa
safari hiyo ndefu ya kutaka kuingia Ikulu ya Marekani.
No comments:
Post a Comment