Vincent Kigosi ‘Ray’.
MGONJWA wa akili akipora nguo zako na kutimka, unachopaswa kukifanya
wewe mwenye nguo ni kuchutama. Ukijiona una mbio sana na kumkimbiza
ukiwa uchi wa mnyama, jamii itakutafsiri wewe ndiye mwendawazimu. Hii
inamaanisha kwamba tunapaswa kuwa makini na aina ya watu wanaotuchokoza.Tazama heshima yako kwenye jamii, muangalie huyo anayekutafuta ubaya, hadhi yake ipoje. Baada ya kupata majibu yenye kujitosheleza, jambo pekee la kufanya ni kuinua mikono na kumshukuru Mjenzi wa Mbingu na Ardhi kisha umlaani shetani kwa sababu mara nyingi hutokea kama malaika wa nuru.
Shetani hana wema, akija kwako lengo lake ni moja tu, kukuharibia, kukusababishia balaa kwenye jamii au kukuchonganisha na Mungu wako. Unaposikia mtu kasema jambo baya kuhusu wewe, usikimbilie kukasirika au kuchukua hatua za mapambano. Anza kwanza kukemea, hilo ni pepo.
Omba Mungu kushinda vita ya nafsi kabla ya kitu chochote. Shinda hisia kila siku kwani hizo ndizo hukupeleka mbali na mara nyingi hukuongoza kuingia vitani. Eti unaamini kuyaacha mambo yapite, utaonekana umeshindwa, kwamba jamii itakuona mnyonge.
Niliona taarifa ya kile ambacho inadaiwa ‘mdada’ anayeitwa Mange Kimambi aliandika kwenye blogu yake akisema Elizabeth Michael ‘Lulu’ hakuhusika na kifo cha marehemu Steven Kanumba ila mhusika nambari moja ni Vincent Kigosi ‘Ray’. Nikajiuliza busara za mhusika.
Kama mtu anaweza kuandika hayo, akijua fika kwamba kifo cha Kanumba bado kinafanyiwa kazi kisheria, ni rahisi kupata jawabu ya kile kilichomo ndani ya kichwa cha ‘mdada’ huyo. Ni msaka shari ya mbali. Zaidi ya hapo ni mshabikia mambo yasiyomhusu na asiyoyajua.
Ray ni nani, Mange yupoje? Nafasi zao zina sura ipi? Majibu ya maswali hayo ni kwamba hawakaribiani hata kwa kulazimisha. Siyo tofauti kama ya usiku na mchana kwa sababu kila moja una uzito wake katika majira bali kuwalinganisha watu hao ni sawa na kufananisha Bajaj na Tingatinga.
Nikiyatafakari malumbano ya Ray na Mange naona ni kupoteza muda. Haiwezekani Corolla Limited ikashindanishwa mbio na Ferrari. Ni haki kwa Ray kumfikisha ‘mdada’ huyo kwenye vyombo vya sheria lakini ushauri wangu kwa staa huyo wa filamu ni kumsamehe, kwani hawalingani.
Ninazo sababu nyingi za kumtaka Ray amsamehe Mange. Mosi ni busara ileile ya kujiweka mbali na Ibilisi. Pili ni kumshauri ajiepushe kuwa daraja la kukuza majina ya watu. Kumpeleka polisi ni sawa lakini pengine hilo ndilo lilikuwa lengo la ‘mdada’ huyo. Pima hoja hii kisha tazama mbele. Nimesema ninazo sababu nyingi, ngoja nizichambue:
Uchunguzi unaonesha kwamba, Mange ni mtu wa shari, mdandia ugomvi, palipo na malumbano ndipo na yeye huweka maskani. Hataki kutulia mahali palipopoa kwa kuona atasahaulika. Anataka atajwetajwe kila siku.
Wanaomjua ni wale wanaotumia muda wao mwingi kwenye mitandao. Hii ndiyo sababu hata vurugu zake huziendesha kwenye blogu na mitandao mingine ya kijamii. Na kwenye eneo hilo, amekuwa akisifika kwa kuchamba watu, ujeuri, nyodo na maneno ya shombo.
Asilimia kubwa ya watu waliopata kuwa marafiki zake amegombana nao. Je, mtu wa namna hii anaweza kukupotezea muda wako Ray? Tazama mbele, una mambo mengi ya kufanya kuliko kusimamisha shughuli zako kwa ajili ya ‘kudili’ na mtu sampuli hiyo.
Hana ngao ya kujivunia zaidi ya kujisifia ana mume wa Kizungu. Dunia hii ya leo, bado mwanamke anaweza kujisifia mwanaume Mzungu? Mpaka hapo hujaelewa Mange ni mtu wa namna gani tu? Je, hujapata picha ya ujazo wa ubongo wake? Kulumbana naye ni kupoteza muda na kujivunjia heshima.
Hata huyo mwanaume wa Kizungu anayemjisifia, habari zinadai hivi sasa picha haziendi. Mdada kang’ang’ania Bongo, mume yupo Dubai. Ndugu yangu Ray, ‘Mtumishi wa Mungu’, mtu anaparurana hata na mtetezi wake namba moja, anayempa jeuri, anaweza kutishika kwako? Angalia, hatua zako zinamfurahisha sana.
Ungekaa kimya angeumia, kawaida yake anapenda akichokoza sehemu, basi mhusika ajibu. Akimnyamazia anakosa amani.
Mange huyu aliwahi kumchokonoa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo. Akamsema sana, akamzushia maneno ya uongo kwenye blogu yake.
Shigongo kwa kutambua nafasi na heshima yake katika jamii, aliamua kumpuuza. Ikafika mahali mdada huyo akakosa cha kuongea, akakaa kimya. Sijui alichokiwaza lakini wenye hekima zetu tulimuona kiroporopo.
Katika hili nimpongeze Shigongo kwa utulivu wake. Kuacha kwake kulumbana na Mange kulimaanisha kweli anatambua heshima yake na thamani yake kijamii. Alithibitisha kwa vitendo kwamba kunyamaza ni hekima. Ray chukua mkondo huo, achana na Mange. Yeye anataka ‘ukomae’ naye ili atengeneze gumzo kwenye blogu na BBM.
Mange huyohuyo alishawahi kumkorofisha wakili maarufu nchini, Sadock Magai. Mwanasheria huyo baada ya kuona mtoto wa kike anazidi kuchezea kichwa chake, akaamua kumchapa. Tuliopo kwenye uwanja wa habari, tunajua kilichotokea. Tafadhali Ray, rudisha moyo nyuma, msamehe huyu dada.
Alivyo Mange ni kwamba hata akiachwa na mpenzi kwake ni vita. Miaka ya nyuma alikuwa na mwanaume Mkenya ambaye baada ya kuona asilimia 85 ya mapenzi yao ni vurugu kuliko mapenzi, aliinua mikono na kumuacha. Mdada huyo hakukubali matokeo.
Mange alimvamia mwanaume huyo usiku, tena akiwa amepumzika na mrembo mwingine mstaarabu (kuliko Mange), mzuri aliyeona anafaa kwa maisha yake, akachoma moto gari lake. Mkenya huyo akamuweka ndani, Mwamvita Makamba ndiye aliyeingilia kati kumsaidia.
Vile Mange alivyo hana shukurani, Mwamvita huyohuyo aliyemtoa mahabusu alipokuwa na kesi ya kuchoma gari la bwana Mkenya, alimgeuka. Kwa kimbelembele chake, siku za hivi karibuni, akachukua picha za nyumba ya Mwamvita na kuzitundika kwenye blogu yake.
Picha hizo zikasababisha gumzo kubwa na baadaye zikamletea Mwamvita matatizo kijamii na kazini. Narudia tena Ray, kama watu ambao ni msaada kwake anawageuka, itakuwaje kwako? Wewe ulikuwa rafiki wa Kanumba, mimi nimekuwa karibu yenu, najua urafiki wenu ulivyo mkubwa licha ya vijidosari vidogo vya hapa na pale.
Wiki iliyopita, Mange huyuhuyu alianzisha vita ya maneno na Mtangazaji wa Radio Times FM, Rose Benard Chitallah. Amemchamba kwelikweli. Hii izidi kusherehesha wasifu wa mdada huyo. Si mtu mwenye staha, anaweza kuzungumza chochote bila kujali, anajidai haogopi lakini si kweli ila ni mtovu wa hekima.
Aliwahi kugombana na aliyewahi kuwa Mtangazaji wa EATV, Teddy Kalonga ‘TK’, matokeo yake Mange akatundika kwenye blogu picha ya mrembo huyo akiwa chooni. Je, Ray bado unahisi unaweza kutumia muda wako kukabiliana na huyu mtu? Acha lipite, kwani hakuna la kudumu hapa duniani, yote yatapita.
Historia ya ukuaji wake, inaweza kutoa picha ni kwa namna gani Mange ni mtu wa chuki. Anapenda kuchukia watu. Na anapoona watu wanafanikiwa, huwachukia. Tazama ‘bifu’ lake kwa Shigongo, Magai, TK, Rose, Mwamvita na wengineo.
Mange akiwa mdogo hakupata mapenzi sahihi ya baba, alilelewa na mama yake katika mazingira duni, Tandika, Dar es Salaam, wakati baba yake akiishi kifahari. Kuishi ki-hohehahe wakati mzazi wa kiume anajiweza, pengine ndiko kulikomfanya awe mtu wa chuki. Ni athari ya kisaikolojia.
Alimchukia baba yake, mama yake wa kambo na watoto wa baba yake, kwani wao walikula ‘bata’, yeye na mama yake wakiishi katika maisha yasiyo na majibu ya baadaye. Baba yake alishatangulia mbele za haki lakini mpaka leo, mdada huyo haivi na ndugu zake pamoja na mama wa kambo. Wamegombania mali mpaka wakafikishana kwenye vyombo vya sheria.
Tuache yote hayo, siku Kanumba alipofariki dunia, Mange alitoa maelezo kwenye blogu yake kwamba haendi msibani kwa sababu hamjui na hakuwahi kuona filamu hata moja ya marehemu. Mtu huyohuyo aibuke na kudai anazo taarifa kuhusu aliyemuua msanii huyo. Huu ni ukorofi, chondechonde Ray usipoteze muda wako. Msamehe.
Mange |
No comments:
Post a Comment