FUNDI umeme Seleman Msaguzi (27), mkazi wa Ubungo Kibangu amekutwa
amekufa chumbani kwake, huku mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema mtu
huyo alikutwa amekufa juzi saa 3.45 asubuhi nyumbani kwake ambapo mwili
wake ulikutwa kitandani umelala.
Alisema chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana na maiti
amehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. Polisi wanaendelea na
upelelezi zaidi.
Wakati huo huo, watu 29 wanashikiliwa Polisi kwa tuhuma za kupatikana na bangi kete 135, misokoto 20 pamoja na puli tatu.
Watuhumiwa hao walikamatwa juzi kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Gongo la Mboto, Keko, Yombo, Kigamboni na Mbezi Makabe.
Kenyela aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Nicholaus Nyagawa (20),
Ally Abdallah (19), Sylvester Mwenda (24), Peter Mathew (27) na wenzao
25.
Watafikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment