Yaliyomo |
Maisha
Steven alianza masomo yake katika shule ya msingi yaBugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.Shughuli za uigizaji
Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90". Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group.Hivi sasa amejibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na amekuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibuni nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu.
Kwa sasa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile ya Dar to Lagos, She is My Sister na nyingine ambazo bado zinajengwa.
Maono Yake
Steven Kanumba ametangaza hivi karibuni nia ya kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.Filamu na Tamthilia Alizotunga
- 1 Tufani ( Johari )
- 2 Gharika
- 3 Baragumu
- 4 Sikitiko Langu
- 5 Johari 2
- 6 Dangerous Desire
- 7 Dar 2 Lagosi
- 8 Cross my Sin
- 9 Village Pastor
- 10 Family Tears
Filamu na Tamthilia Alizoigiza
- 1 Jahazi ( Tamthilia )
- 2 Dira ( Tamthilia )
- 3 Tufani ( Johari )
- 4 Gharika( Tamthilia )
- 5 Baragumu( Tamthilia )
- 6 Sikitiko Langu ( Filamu )
- 7 Johari 2 ( Filamu )
- 8 Dangerous Desire ( Filamu )
- 9 Dar 2 Lagosi
- 10 Riziki (film) ( Filamu )