Watoto yatima wakiwa na Uwoya, Mariamna Krish.
Uwoya akikabidhi msaada wake kwa katibu mkuu wa kituo hicho cha CHAKUWAMA.
ICON wa filamu nchini, Irene Uwonya jana usiku wa Mei 8 aliandaa
bonge la siku ya kuzaliwa mtoto wake wa kiume, Krish Ndikumana, akiwa
ametimiza umri wa mwaka mmoja tangu azaliwe.Uwoya akikabidhi msaada wake kwa katibu mkuu wa kituo hicho cha CHAKUWAMA.
Krish ni mtoto wa mwanasoka raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’.
Sherehe hiyo ilifanyika katika kituo cha watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza-Mori jijini Dar.
Akizungumza na mtandao huu, mama wa mtoto huyo, Irene Uwoya, alisema amefarijika sana kufanya sherehe ya mwanaye akijumuika na watoto yatima kwani ameona ni moja ya kuwahakikishia watoto hao kuwa jamii inawajali.
“Sikutaka sherehe hii ya mwanangu niifanye katika ukumbi na kualika watu wengi ili waje kunywa na kula huku nyinyi watoto wenzake mkiwa mpo, kwani hiyo haitokuwa vizuri kwa upande wangu,” alisema Uwoya.
(by global publishers.)
No comments:
Post a Comment