Monday, May 28, 2012

MWACHENI MUNGU AITWE MUNGU!!


Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa hospitalini nchini India.
Sajuki akiwa amepumzika, pembeni ni mkewe Wastara Juma.

HEBU mwacheni Mungu aitwe Mungu! Hatimaye habari njema kutoka katika Hospitali ya Saifee iliyopo jijini Mumbai, India anakotibiwa staa wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ zinatia faraja kwa Watanzania, Ijumaa Wikienda linakupa stori ‘exclusive’ kutoka nchini humo.
ANYANYUKA KITANDANI, AONGEA
Habari hizo njema zinaeleza kuwa Sajuki aliyeambatana na mkewe, Wastara Juma na kaka yake, hatimaye ameweza kunyanyuka kitandani na kuongea tofauti na siku aliyoondoka Bongo na mwanzoni alipofikishwa hospitalini hapo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu, Wastara alisema Sajuki alikuwa amepata nafuu na hali siyo mbaya kwani alikuwa na uwezo wa kuzungumza hivyo akampa simu ili azungumzie afya yake yeye mwenyewe jinsi anavyojisikia.
SAJUKI LAIVU
Sajuki alipopewa simu alianza kwa kuwashukuru wale wote wanaomuombea dua na kujitolea kwa hali na mali ili kuokoa uhai wake.
“Namshukuru sana Mungu naendelea vizuri. Nilichukuliwa vipimo na nikabainika kuwa na uvimbe mwingi sehemu mbalimbali tumboni.
“Madaktari walibaini kuwepo kwa uchafu kwenye mapafu. Mwanzoni waligundua nina tatizo la kupumua na kukaukiwa damu.
“Wamelishughulikia hilo kwanza na hapa nilipo nimezungukwa na madawa, kwa kweli najisikia nafuu,” alisema Sajuki kwa sauti ya kukwaruza.
MADAKTARI
Sajuki alisema alipokelewa vizuri lakini kabla ya kuanza matibabu ya uvimbe tumboni, madaktari walilazimika kumtibu kwanza tatizo la damu na pumzi hivyo matibabu ya kilichompeleka hospitalini hapo (uvimbe) yakawekwa pembeni.
WASTARA ATIA NENO
Kwa upande wake, Wastara alisema kuwa Sajuki alipaswa kupatiwa matibabu kwa wiki mbili ndipo warejee nyumbani lakini kwa hali halisi inaonekana watakaa zaidi kwani tayari wiki mbili zimekatika.
MATIBABU YAANZA
Wastara alisema kuwa baada ya kumalizika kwa tatizo la pumzi na kupungukiwa damu, madaktari wameanza vipimo vya tatizo la uvimbe na kusisitiza kuwa uzi ni uleule wa kumwombea mumewe ili arejee katika siha njema.
TUMEFIKAJE HAPA?
Sajuki alianza kusumbuliwa na uvimbe mwaka jana ulioanzia mkononi na baadaye ndani ya mwili kwenye ini na sasa madaktari wanasema siyo kwenye ini tu bali na sehemu nyingine tofauti za tumboni.
NENO
Kama alivyosema Wastara, tuzidi kumuombea dua Sajuki ili arejee katika ulingo wa filamu aendelee kutuelimisha na kutuburudisha tunapokuwa majumbani mwetu.

Thursday, May 17, 2012

Baadaya Kanumba,Eeeh Mafisango Tena!!!Nani atafuata?


Rafiki wa karibu na marehemu ambaye amenusurika kwenye ajali hiyo (kulia) akilia kwa uchungu.
Mchezaji wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ (kulia),  akiwa wamekaa kwa huzuni na  wenzake.
Boban akilia kwa uchungu.…

Rafiki wa karibu na marehemu ambaye amenusurika kwenye ajali hiyo (kulia) akilia kwa uchungu.
Mchezaji wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ (kulia),  akiwa wamekaa kwa huzuni na  wenzake.
Boban akilia kwa uchungu.
Mchezaji wa Moro United, Jackson Chove, akiwa na huzuni.
Waombolezaji  ambao ni mashabiki zake wakilia kwa uchungu.
Kifo cha kiungo mkabaji wa timu ya Simba, Patrick Mafisango,  kilichotokea leo alfajiri maeneo ya Veta-Chang’ombe  jijini Dar es Salaam baada ya kupata ajali ya gari,  kimewahuzunisha watu  wengi ambao  walikusanyika nyumbani kwa mchezaji mwenzake, Emannuel Okwi, maeneo ya Bora-Keko ambako taratibu za msiba zinafanyika huku wakilia kama watoto.

40 ya Kanumba Giza latanda!!!


Marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’.
Mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa.
Baba mzazi wa marehemu Kanumba, Mzee Charles Kanumba.…
Marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’.
Mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa.
Baba mzazi wa marehemu Kanumba, Mzee Charles Kanumba.
Sehemu ya umati uliohudhuria msiba wa marehemu Kanumba.
Issa Mnally na Shakoor Jongo
LEO ni siku ya arobaini tangu kifo cha aliyekuwa nyota wa sinema za Bongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’ lakini giza nene linaonekana kuigubika shughuli hiyo kufuatia tamko la mama wa marehemu, Amani linakuja na habari kamili.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu juzi Jumanne, mama wa marehemu, Flora Mtegoa alisema ni kweli arobaini imefika lakini hajui kinachoendelea ila itafanyika Mei 20, 2012.
TAMKO LA MAMA
Mama Kanumba alikuwa akijibu swali la kipaparazi lililomtaka afafanue kama mkusanyiko wa arobaini ya marehemu utakuwepo au kila mtu atakuwa kivyake.
“Nimeambiwa itafanyika tarehe 20 mwezi huu lakini zaidi ya hapo sijui chochote kile kinachoendelea mwanangu,” alisema mama huyo kwa sauti iliyojaa unyenyekevu.
HABARI NDANI YA TASNIA YA SINEMA
Amani lilizungumza pia na mmoja wa wasanii wa filamu za Kibongo ambaye hakupenda jina lake liwekwe wazi. Yeye alikuwa na haya ya kusema:
“Ilibidi arobaini yake
ifanyike Mei 17 (leo) lakini kila tukiulizia tunaambiwa mipango bado haijakamilika, mipango gani hiyo kama fedha zilipatikana nyingi sana katika rambirambi.
“Wanaona hasara kuzitoa kwa ajili ya kununulia vifaa vya arobaini?”
Aidha, msanii huyo aliitaka kamati ya maandalizi ya arobaini hiyo (kama ipo) kutoifanya kienyeji na kushauri kuwa inabidi itangazwe ili watu wahudhurie kwa wingi kama siku ya mazishi.
“Kinachoonekana wanataka kufanya shughuli bora ifanyike, watakuwa wameharibu sana. Wakifanya shughuli kubwa pengine hata rais au mawaziri na wabunge wanaweza kuhudhuria,” alisema msanii huyo.
MANENO YA JB
Msanii Jacob Steven JB, Mwenyekiti wa Bongo Movie, alipoulizwa na gazeti hili siku ya Jumanne (juzi) alisema hajui lolote kuhusu arobaini hiyo.
Akasema: “Kwa taarifa nzuri labda muulize Gabriel Mtitu ‘Mtitu Game’ (aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maziko), yeye atakuwa anajua lolote.”
SAUTI YA MTITU GAME
Amani lilimtwangia simu Mtitu Game na kumuuliza kama anajua lolote kuhusu kuwepo kwa arobaini ya marehemu Kanumba.
“Aaa, yeah! Arobaini imeangukia Alhamisi, siku ya kazi. Kwa hiyo familia ikaona ifanyike Mei 20, mwaka huu ambayo itakuwa Jumapili,” alisema Mtitu.
Amani: “Kwa hiyo ishu itakuwaje?”
Mtitu: “Aaa! Kutakuwa na ibada pale Kanisa la AIC Chang’ombe, halafu baadaye wanandugu watakusanyika nyumbani kwa marehemu (Sinza) kwa ajili ya chakula cha pamoja.”
Amani: “Hakuna mwito kwa mtu yeyote atakayetaka kuja?”
Mtitu: “Sijalijua hilo.”
BABA KANUMBA NAYE
Baada ya mawasiliano yote hayo, Amani lilimpigia simu baba mzazi wa marehemu, Mzee Charles Kanumba na kumuuliza kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa arobaini ya mwanaye.
Akafunguka: “Sijajua, ila lazima iwepo.”
Amani: “Huku mama wa marehemu naye anasema hajui lolote, wewe unasema hujajua.”
Baba: “Yeye (mama Kanumba) kusema hajui lolote ni janja ya nyani tu. Mimi najiandaa kuja huko siku mbili hizi, nikifika kila kitu kitajulikana.”
CHANZO CHA YOTE
Chanzo cha yote haya ni simu zilizoanza kumiminika kwenye Ofisi za Global Publishers, wasomaji wa Dar na mikoani wakiulizia shughuli hiyo itafanyikia wapi ili wahudhurie.
Juma Makala wa Mwanza, alitaka kujua siku na mahali ili aweze kufika baada ya kushindwa kuhudhuria mazishi ya marehemu.
“Jamani naitwa Juma Makala, niko Mwanza. Hivi hii arobaini ya Kanumba ni lini? Nahisi imekaribia. Na itakuwa wapi? Kwa sababu sikuweza kuhudhuria kwenye mazishi sasa nilitaka kujua ili niweze kufika.”
Amani lilimjibu aendelee kufuatilia magazeti ya Global atajua ni lini.
Mama Mage wa Kinyerezi, Dar yeye alisema alitaka kwenda Afrika Kusini kwa matibabu lakini amesitisha kusubiri arobaini ya Kanumba lakini hajui itakuwa lini.
Amani lilimuomba kuendelea kusoma magazeti ya Kampuni ya Global Publishers ili kujua ni lini na wapi.
NENO LA MHARIRI
Arobaini ya Kanumba imefika, kama ni Mei 20 ni vyema watu wakasubiri tamko maalum la familia ambalo naamini litaweka wazi hata wenye sifa za kuhudhuria.

Sunday, May 13, 2012

Man city bingwa England



Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany akiwa amenyanyua juu kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kuwafunga QPR katika mechi ya leo.Mshambuliaji wa  Manchester City, Sergio Aguero (jezi namba 16) akiifungia timu yake bao la tatu na la ushindi dhidi ya Queens Park Rangers katika mechi iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, England. Manchester City wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya mabao na Manchester United.
 (Picha zote kwa hisani ya Getty Images)…


Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany akiwa amenyanyua juu kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kuwafunga QPR katika mechi ya leo.Mshambuliaji wa  Manchester City, Sergio Aguero (jezi namba 16) akiifungia timu yake bao la tatu na la ushindi dhidi ya Queens Park Rangers katika mechi iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, England. Manchester City wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya mabao na Manchester United.
 (Picha zote kwa hisani ya Getty Images)

Thursday, May 10, 2012

KINACHOMTESA LULU!!





ITAKUMBUKWA kuwa Jumatatu iliyopita, mshitakiwa katika kesi ya kifo cha staa wa sinema za Kibongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alitupiwa ombi lake la kutaka mahakama imtambue kuwa ana miaka 17 badala ya 18 ili kesi hiyo iendeshwe kwenye mahakama ya watoto.

Kesi hiyo ambayo iliunguruma Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mawakili wanaomtetea mshitakiwa huyo wakiongozwa na Kenedy Fungamtama waliwasilisha cheti cha kuzaliwa cha mlalamikiwa wao kinachoonesha ana miaka 17.
Hoja hiyo ilitupiliwa…



ITAKUMBUKWA kuwa Jumatatu iliyopita, mshitakiwa katika kesi ya kifo cha staa wa sinema za Kibongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alitupiwa ombi lake la kutaka mahakama imtambue kuwa ana miaka 17 badala ya 18 ili kesi hiyo iendeshwe kwenye mahakama ya watoto.
Kesi hiyo ambayo iliunguruma Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mawakili wanaomtetea mshitakiwa huyo wakiongozwa na Kenedy Fungamtama waliwasilisha cheti cha kuzaliwa cha mlalamikiwa wao kinachoonesha ana miaka 17.
Hoja hiyo ilitupiliwa mbali na mawakili wa upande wa mashitaka waliokuwa wakiongozwa na mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama hiyo, Elizabeth Kaganda ambaye alisema cheti hicho kina dosari kadhaa.
Naye hakimu aliyesikiliza kesi hiyo, Augustine Mmbando alisema mahakama hiyo itaendelea kuutambua umri alioutaja mshitakiwa wakati akitoa maelezo yake polisi hadi pale kesi yake itakapoanza kusikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.
DOSARI YA KWANZA
Jina la mshitakiwa lilisomeka ni Diana Elizabeth Michael badala ya Elizabeth Michael. Mwendesha mashitaka huyo alisema jina hilo ni geni mahakamani hapo.
DOSARI YA PILI
Kaganda alisema mapungufu mengine ni cheti hicho kugandishwa kwenye nailoni (lamination) jambo ambalo halitakiwi kwenye uhifadhi wa vyeti.

KINACHOMTESA LULU
Kwa mujibu wa mazungumzo ya watu na wanasheria kadhaa, Lulu kwa sasa anateswa na mazingira aliyokuwa akiishi ambayo kwa sehemu kubwa yanapingana na umri unaotajwa.
Endapo msanii huyo angekuwa si maarufu, hakuna mtu ambaye angeibua utata wa umri wake kwa vigezo au ushahidi kama ilivyo sasa.
Kwa mujibu wa Kaganda, wakati akitoa maelezo kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar baada ya kukamatwa, Lulu alisema ana miaka 18 na aliambiwa ayapitie mara kadhaa maelezo yake kabla ya kuanguka sahihi.
Akizungumza baadaye, afisa mmoja mwandamizi wa mahakama hiyo alimwambia Kaganda:
“Wanasema Lulu ana umri wa miaka 17, mbona huwa anaonekana akiendesha magari, alipataje leseni akiwa na umri wa chini ya miaka 18?”
Kaganda: “Si ndiyo hapo sasa!”

SHEREHE YA BETHIDEI
Pamoja na malumbano hayo makali juu ya umri wa Lulu ndani ya mahakama hiyo, nje nako minong’ono ilishamiri. Sherehe yake ya kutimiza miaka 18 iliyoripotiwa kwenye vyombo vya habari, Aprili 2011 nayo ilitajwa.
“Halafu huyu Lulu si alishafanya bethidei ya kutimiza miaka 18 mwaka 2011, tena hata magazeti na kwenye mitandao waliandika,” alisema mtu mmoja nje ya mahakama hiyo.
“Nini kufanya bethidei, kwenye kipindi cha Mkasi alipohojiwa na Salma Jabir wiki moja tu kabla ya kifo cha Kanumba, Lulu alikiri ana miaka 18. Lakini pengine kweli, labda ni utoto ndiyo maana hana uhakika na umri wake,” alisema mwingine.

KUJIRUSHA KLABU
Aidha, minong’ono hiyo pia ilisikika ikijadili suala la msanii huyo kuwahi kuripotiwa (Machi 2011) kwamba alipigwa marufuku na mameneja wa klabu kubwa za usiku za jijini Dar kutokana na kuwa na umri mdogo, lakini baadaye mwenyewe akasema ‘amuone huyo wa kumkataza kuingia klabu.’
Wafuatiliaji hao walisema baada ya kutoa tamko hilo ndipo miezi michache mbele, Lulu akaangusha bethidei ya nguvu kwamba alitimiza miaka 18 hivyo alikuwa huru kuingia klabu kujirusha.
Walisema katika kujirusha kwake klabu, alisharipotiwa kuwa aliwahi kulewa chakari hadi nguo zikamvuka.

MADAI YA UHUSIANO NA ALI KIBA
Wapo pia waliokumbusha habari iliyowahi kuandikwa kwenye gazeti la Risasi la Septemba 4, 2010 ikiwa na kichwa cha kisemacho; ALI KIBA KUFIA JELA…endapo itathibitika Lulu ni mtoto mdogo (chini ya 18).
Katika habari hiyo, ilidaiwa kuwa, msanii huyo wa Bongo Fleva alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye iliaminika ana miaka chini ya 18.
MAMA MZAZI ATETWA
Mama mzazi wa Lulu ameendelea kubebeshwa lawama kuhusu utata huo. Wengi walisema wakati mtoto wake anafanya bethidei kutimiza miaka 18 aliona au kusoma kwenye magazeti, kwa nini asipinge kama alijua amedanganya?
“Mama anasema mtoto wake ana miaka 17, siku zile anafanya bethidei mwanaye huyo alisema ametimiza miaka 18 kwa nini asipinge, ameona yaliyotokea sasa?” alihoji Mwantumu, mkazi wa Upanga, Dar.

MEZANI KWA MHARIRI
Amani linaamini yote ni maneno yanayosemwa, mahakama zetu zipo imara na zenye kufuata sheria, zitaendesha kesi hiyo kwa mujibu wa sheria na si maneno ya watu.

Wednesday, May 9, 2012

Mtoto Krish akifurahia jambo.
Muigizaji Tino akiwasha mishumaa.
Baadhi ya watoto yatima wakiimba wimbo wa ‘Happy Birthday’.
Krish na mama yake wakizima mishumaa.…
Mtoto Krish akifurahia jambo.
Muigizaji Tino akiwasha mishumaa.
Baadhi ya watoto yatima wakiimba wimbo wa ‘Happy Birthday’.
Krish na mama yake wakizima mishumaa.
Krish akisaidiwa na mama yake kukata keki.
Uwoya akimlisha kipande cha keki mtoto wake.
Uwoya akitoa hotuba.
Watoto yatima wakiwa na Uwoya, Mariamna Krish.
Uwoya akikabidhi msaada wake kwa katibu mkuu wa kituo hicho cha CHAKUWAMA.
ICON wa filamu nchini, Irene Uwonya jana usiku wa Mei 8 aliandaa bonge la siku ya kuzaliwa mtoto wake wa kiume, Krish Ndikumana, akiwa ametimiza umri wa mwaka mmoja tangu azaliwe.
Krish ni mtoto wa mwanasoka raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’.

Sherehe hiyo ilifanyika katika kituo cha watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza-Mori jijini Dar.

Akizungumza na mtandao huu, mama wa mtoto huyo, Irene Uwoya, alisema amefarijika sana kufanya sherehe ya mwanaye akijumuika na watoto yatima kwani ameona ni moja ya kuwahakikishia watoto hao kuwa jamii inawajali.

“Sikutaka sherehe hii ya mwanangu niifanye katika ukumbi na kualika watu wengi ili waje kunywa na kula huku nyinyi watoto wenzake mkiwa mpo, kwani hiyo haitokuwa vizuri kwa upande wangu,” alisema Uwoya.


(by global publishers.)

BASI LA ABIRIA LATEKETEA!

Basi la kampuni ya Muro Investment, lenye namba za usajili T820BEY lillilokuwa likitokea Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea  kabisa maeneo ya Maseyu, Mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku  wa Mei 8, 2012, haikusababisha madhara kwa abiria isipokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto
 Magari yakipita pembeni ya basi hilo lililokuwa likiteketea kwa moto na hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuzima moto huo ulioliteketeza basi hilo…