KAMA nyota wa Yanga walidhani ujio wa kocha mpya, Tom Saintfiet, utakuwa starehe tupu wamejidanganya kwani Jerry Tegete na Athumani Iddi Chuji wamekuwa wa kwanza kuonja joto ya jiwe ya Mzungu huyo kwenye mazoezi ya jana Jumatatu.
Mbelgiji huyo alidhihirisha si mtu wa mzaha baada ya kutoa adhabu ya kupiga `push up' 10 kwa kila mmoja wa wawili wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Saintfiet alikasirishwa na kitendo cha nyota hao kutokuwa makini kwenye mazoezi.
Baada ya kuwaadhibu akina Chuji, Saintfiet aliwaambia wachezaji kutofanya mzaha wakati wa mazoezi na kuwataka wawe wakakamavu na makini wakati wote kama wanajeshi.
"Ninataka kila mchezaji afuatilie kwa makini mazoezi na hii yote ni kwa manufaa ya timu. Hakuna mtu, ambaye yuko juu ya timu. Muwe kama wanajeshi," alisikika Saintfiet akiwaambia wachezaji hao wakati wa mazoezi hayo.
Katika hatua nyingine, Mnyarwanda Haruna Niyonzima amekoshwa na staili ya ufundishaji wa kocha huyo.
�Kila mchezaji amefurahishwa na staili ya ufundishaji wa Saintfiet, nafikiri tumepata bonge la kocha, naamini ataibadilisha Yanga na kucheza soka la kisasa,� alisema Niyonzima.
No comments:
Post a Comment