Thursday, September 6, 2012

Dotynta Amvuta Kaseba.


Husna Poshi 'Dotnata'
MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu za Swahiliwood, Husna Poshi 'Dotnata', yupo katika maandalizi ya filamu mpya ambayo ameshirikiana na mpiganaji wa ngumi za mateke, Japhet Kaseba pamoja na mkewe.

"Ni filamu ya kipekee, itakuwa bomba sana wenyewe mtaikubali," alisema Dotnata.

"Ni kweli mara nyingi watu wanaandaa filamu za mapigano lakini kuna sehemu zinakosewa kwani huwa zinatumia upiganaji wa kifilamu.

"Lakini katika kazi hiyo mpya mtakutana na mtu mwenye fani yake. Kwa kilichofanyika mpaka sasa ninajivunia ubora wa filamu hiyo.

"Siitaji jina kwa sasa, lakini mtaipata muda si mrefu ujao, kaeni mkao wa kula."

Kaseba ni mpinzani mkubwa wa bongia mwingine wa ngumi za mateke, Seba, ambaye yeye aliingia katika tasnia ya filamu kitambo.

Akizungumzia hilo, Kaseba, amesema alikuwa akisita kuingia katika filamu kutokana na fani hiyo kuwa chini mno nchini, lakini sasa ameridhika kuwa angalau inapiga hatua.

No comments: